Sunday, January 27, 2013

Kongamano la Kiswahili lafana...

Ni tarehe 26,Januari 2013,ni siku ya kumbukumbu kwa Wanachuo wa Teku,hususani wale wanaosoma somo Kiswahili kama sehemu ya Kozi zao.........ama hakika ule msemo wa shughuli haina udogo....ulijitokeza...lakini hatimaye shughuli ilipendeza na hata kufana.....wapongezwe wale walioandaa na kufikia mafanikio.Zifuatazo baadhi ya picha zenye kuonesha matukio machache katika Kongamo hilo. Karibu sana!!!!!

Aliyesimama ni Mama Mboya aikiwa anasema chochote kabla ya kumkaribisha Profesa Msanjila kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam(UDSM) ili kutoa mada iliyoandaliwa siku hiyo.




Mama Mbayo akiwa yupo kidijitali{kijijiti}zaidi.....huku akichukua matukio mbalimbali ya kongoma.....hongera sana Mama kwa kuwaongoza vijana kimtandao.


Hongera sana dada....!!!!haya ni baadhi ya maneno yaliyokuwa yakisemwa na washiriki wa kongamano....ni mmoja kati ya washiriki waliotoa burudani siku ya kongamano.......ailitoka Kimpotompoto.....


hawa ni vijana...ambao walileta raha katika kongamano hilo....kwa kutoa maagizo na vichekesho vyenye mafundisho ya kutosha.....hakika vijana wanavipaji...vinatakiwa kuendeleza.

kaka Mgeta nae alikuwepo na kufuatilia Kongamano kwa karibu sana.......pamoja dada wa Bel,akiwa amevalia tenge kama la Mama Kikwete.

B
Baadhi ya washiriki wa kongamano walipiga picha ya pamoja na profesa Msanjila akiwa na mkewe pamoja na muhadhiri Sigila kama mkuu wa idara ya lugha.

Profesa akiwaaga wanakongamano.............kwaheri baba......ufike salama Dar es salaam.

21 comments:

  1. Kwa kweli kongamano lilifana sana.Sasa nimepata uelewa zaidi kuhusu Sera ya matumizi ya Lugha Tanzania. SAMSON BARAKA

    ReplyDelete
  2. nafikiri ni wakati wa kuona ukweli uko wapi juu ya lugha yetu ya kiswahili tumekuwa watumwa mpaka katika lugha yetu. jamani tubadilike tuwe wanamapinduzi tuitetee lugha hii bora kabisa barani Afrika. AHMED SALUM

    ReplyDelete
  3. kweli ilifana. tunaomba makongamano mengine yaandaliwe. MWAKANYAMALE PENDO

    ReplyDelete
  4. ni vyema sn....................................!!!!

    ReplyDelete
  5. jambo la kufurahisha na kutia matumaini.....,hongera kwa kitivo cha lugha TEKU.

    ReplyDelete
  6. kwa kongamano hili napendekeza kiswahili iwe lugha ya kufundishia katika viwango vyote vya elimu ili tuzidi kuienzi NYAMBO EKLESIA.

    ReplyDelete
  7. Hakika kongamano limetuzidi kitambulisha chuo cha TEKU kitaaluma. hivyo tuzidi kukienzi kiswahili kama lugha ya Taifa.

    ReplyDelete
  8. Hakika kongamano limekitambulisha chuo cha TEKU kitaaluma. hivyo yuiendeleze lugha ya kiswahili. MWAKWENDA JENI

    ReplyDelete
  9. Kongamano limeniwezesha kujua lugha yetu ya kiswahili. na pia umuhimu wa lugha zote mbili katika ulimwengu wa sayansi na teknolojia. JOSHUA ANGABILE

    ReplyDelete
  10. Hakika kongamano limenisaidia sana kuniongezea maarifa zaidi juu ya lugha yetu adhimu ya KISWAHILI.

    ReplyDelete
  11. Kwa kweli kongamano limenisaidia kutambua nafasi ya lugha ya kiswahili. Nawashukuru wote walioshiriki kuandaa kongamano hili. MWALIZI.S. LOYCE TEKU/BAED/10602

    ReplyDelete
  12. Nawatakia maandalizi mema ya mitihani pia msimsahau mungu wenu. KOMBA EDWARD A,

    ReplyDelete
    Replies
    1. PIA NAMI NAKUTAKIA MTIHANI MWEMA. KAMUA TUTOKE ILI TUJE KUVAA JOHO MWEZI WA KUMI. AHMED SALUM

      Delete
  13. Tuwakumbuke na wenzetu wanaoumwa katika kipindi hiki cha mitihani Mungu awape nguvu waweze kupona na kufanya mitihani vizuri.KIMARO, JACKLINE B.

    ReplyDelete
  14. tuwaombee wenzetu waliokosa ada waweze kufanya mitihani. ANYINGISYE FEBI

    ReplyDelete
  15. MUNGU AWABARIKI KATIKA MITIHANI YENU. PILLA ANUSIATA

    ReplyDelete
  16. Hopely I'm among those who wish you all the best in your upcoming "UNIVERSITY EXAMINATION". May all GOD's blessing be with you, Have success preparation, particularly to TED 501.
    GREAT.

    CHACHA JAMES. TEKU/BAED/10160

    ReplyDelete
  17. ni kweli tumejifunza na wapi tunaelekea tujitathimini na lugha yrtu ya kiswahili ni lugha bora.MWAIJANDE ELIZABETH.

    ReplyDelete
  18. nami naunga mkono juu ya hili tuthamini lugha yetu jamani. MWAKATIKA JAMES. TEKU/BAED/10581

    ReplyDelete