Monday, January 28, 2013

Fikilia kwa makini na Uchangie juu ya Kauli hizi...........

 Imeonekana kuwa sera ya lugha ya nchi yetu (Tanzania) ni dhaifu,inahitaji kuboreshwa. Kwa mfano sera ya lugha ina mpango lugha mmoja tu wa Kiswahili kuwa lugha ya kufundishia na kusahau lugha ya Kiingereza, Kifaransa na zinginezo. Hii inatokana na changamoto za Utandawazi, kwahiyo sera ya lugha ni lazima ije na utekelezaji wa utumizi wa lugha zingine kama zilivyotajwa hapo juu.


 "...................kwahiyo Rais wa nchi ni lazima aunde Tume ya Elimu ili ichunguze mfumo mzima wa elimu na gharama zake na utekelezaji wake.Baada ya hapo Tume hiyo ije na mpango unaotekelezeka wa kimaendeleo.............".(Profesa Y.P Msanjila)


Ukiwa kama mdau wa Lugha ya Kiswahili na Sera zake,unatoa mchango gani katika hitimisho hilo hapo juu.Karibu tushiriki.

41 comments:

  1. serekali inatakiwa kuunda tume ya utekelezaji wa sera ya lugha na sio kuunda tume ya kuunda sera ya lugha bila utekelezaji
    KALULU ZAINABU

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ni kweli lakin hapa kwetu Tanzania itabaki mbwembwe tu maana vyote hivyo wanavijua sema wanapotezea kwani hakuna mtoto wa mkubwa anayepata athari kwendana na sera hiyo,watoto wao nje kwa sna kimasomo kwa hiyo maumivu kwetu,sijui tufanye nini ili tuondokane na hili tatizo maana hata ikitolewa hoja mbungeni na kambi ya upinzani utawaona wako kinyume sijui wanataka tuandame tu kila siku watafyatue mabomu ya machoz?
      SAKTAY JOSEPH
      TEKU/BAED/10769

      Delete
  2. Nina kubaliana na kauli ya Profesa Msanjila kwasababu bila ya kuwa na taarifa muhimu zitakazosaidia kufahamu suala zima la lugha na gharama zake pamoja na mahitaji ya jamii ni kazi bule kuwa na sera ya lugha isiyokidhi mahitaji ya jamii na maendeleo kwa ujumla......Lugha ni chanzo muhimu cha maendeleo kwa nchi kama Tanzania ili kurahisisha mawasiliano baina ya wanajamii na hata kuwasiliano na watu mbalimbali duniani.

    Ephron Jeremia,Teku/bel/ 10928

    ReplyDelete
    Replies
    1. lugha bila ya kuwa na sera ni sawa na kuwa na gari lisilokuwa na injini itakayosaidia gari husika kutembea.........nakubaliana na Profesa Msanjila kwa hitimisho lake.
      Kamwela Erasto,Teku/Bel/10954.

      Delete
    2. Ni sawa na kuwepo na gari lisilo na hata usukani utakao saidia gari hilo kuwa na mwongozo mzuri wa njia ili gari husika lifike katika safari yake salama.....ni kweli Profesa amegundua njia sahihi kwa kuiokoa lugha yetu na hata kimatumizi yake ili watanzania tujivunie lugha ya kiswahili na hata tufanikiwe katika maendeleo ya kijamii katika nyanja zote.
      Maberi Immaculata,Teku/Bel/10972.

      Delete
    3. Hakika Profesa Msanjila amegundua njia sahihi ya jamii ya kitanzania inatakiwa kuelekea....hakuna budi serikali yetu kutafuta dawa ili kuweza kutibu tatizo lilokuwepo katika jamii yetu ya kitanzania yaani kwa kuwa na Tume kwanza na baadae tuwe na sera husika ya lugha.
      Sleyyum Abdul-Salami,Teku/Bel/101070.

      Delete
    4. Tume itakayoundwa na Rais wa nchi itakuwa suluhisho pekee la kufikia muafaka wa kuwa na sera ya lugha iliyokuwa na njia mbadala ya kuiwezesha lugha ya kiswahili kuwa kichocheo cha maendeleo kwa wananchi au jamii ya kitanzania huku ikiaminika kuwa tupo katika ushindani wa kuifanya nchi yetu kuwa yenye kuendelea na sio kubaki nyuma kimaendeleo katika nyanja zote za maisha.
      Kateule Joyce,Teku/Bel/10956.

      Delete
  3. NINKUBALIANA NA PRO MSANJIRA KUWA TATIZO SI KUTUMIA KISW KAMA LUGHA YA KUFUNDISHIA, ILA KUNA MIPANGO GANI ILIYOANDALIWA ILI NA LUGHA NYINGINE ZIFANYE KAZI YAKE? HIVYO SERIKALI INATAKIW KWANZA IANDAE MPANGO MZURI UTAKAOIFANYA LUGHA HII KUTUMIKA KATOKA NYANJA ZOTE.

    (SESEME SHABANI A)

    ReplyDelete
    Replies
    1. BIG UP WOTE MNAOTAMBUA UMUHIMU WA KISWAHILI

      Delete
  4. ILI KUIBORESHA LUHGA YA KISWAHILI KWANZA WAZAWA WA LUGHA HII HAWANA BUDI KUITHAMINI KATIKA HALI YOYOTE ILE ILI KUWEZA KUKIENZI POPOTE PALE ULIMWENGUNI
    KOMBA MATHEW TEKU/BAED/O9213.

    ReplyDelete
  5. NI WAZI KUWA LUGHA YA KISWAHILI INAJITOSHELEZA KIMATUMIZI,KWANI INAWAFAA WATUMIAJI WENGI(WATANZANIA) KATIKA SHUGHULI ZA MAWASILIANO.HIVYO NI BORA IKAWA LUGHA YA KUFUNDISHIA SHULENI NA VYUONI,KATIKA SHUGHULI ZA BIASHARA, MAOFISININA KATIKA SHUGHULI ZA KITALI, ILI KUONYESHA UZALENDO WA TAIFA LETU KWANI LUGHA HII NI KITAMBULISHO CHA TAIFA LETU.
    PANJA SOPHIA.TEKU/BAED/10729.

    ReplyDelete
    Replies
    1. NI KWELI KAMA TUKITUMIA KISWAHILI KATIKA NYANJA ZOTE BASI KITATHAMINIKA KIMATAIFA. LUGHA YA KISWAHILI NI TAMU KIMATUMIZI. TUZIDI KUDUMISHA UTAMADUNI WETU WATANZANIA.
      mwakanyamale pendo.
      TEKU/BAED/10579

      Delete
    2. hapo umeongea la maana kwani kuna wengi wanaoikana kiswahili na kuona ni lugha ya watu wa chini wakati leo hii ndo imeshika kasi na imekuwa na mshiko kwa wengi hata kwa wazungu mnaotamani lugha yao
      SAKTAY JOSEPH B
      TEKU/BAED/10769

      Delete
  6. EDUCATION MEDIA AND TECHNOLOGY COURSE INFLUENCE US TO BE OPEN IN LEARNING THROUGH THEORETICAL AND PRACTICAL HENCE TO BE USEFUL IN TEACHING USING MEDIA.THIS IS DUE TO EFFORT MADE BY OUR COURSE LECTURER.

    MANUEL REHEMA.TEKU/BEL/10977

    ReplyDelete
    Replies
    1. Exactly your comment is significant simply because up to date number of teachers attended TED 501 are familiar with teaching using MEDIA TECHNOLOGY including I.So big hands and congratulations to the course instructor and I declare that we are now current teachers.
      GEORGE JOSEPH N.
      TEKU/BAED/10219

      Delete
    2. jamani tuko kwenye sera ya lugha, MR COMENT

      Delete
  7. Although use of technology in the classroom interaction is very difficult by the most teachers in developing countries,but no way out we have to use it as the changes taking place in education system in the world,for example the millennium development goals that by 2020-2025 every teacher should have to go for the computer course
    By Saktay Joseph
    TEKU/BAED/10769

    ReplyDelete
    Replies
    1. bro life of now day we are in digital so your right we modern teacher we must have computer technology. AHMED SALUM. TEKU/BAED/10112

      Delete
  8. But this depends on the working environment of the teacher.TEKU/BAED/10850.

    ReplyDelete
  9. MGAYA JOSEPH R BEL 10991
    kiukweli mawazo ya kuhusu sera ya lugha yapo sahihi iv chukulia tunaongea kiawahili tu kiswahili tu,tungewezaje kuwasiliana na watu wa nje,hivyo sera ya lugha tulionayo iko sawa kabisa na ninivyoona ime weza ku weka usawa katika ujuz na utumiz wa lugha mbili

    ReplyDelete
    Replies
    1. MGAYA HAPANA KAKA MBONA WACHINA WANATUMIA LUGHA YA KWAO NA WAMEENDELEA SANA KULIKO SISI TULIO KATIKATI YA LUGHA MBILI NA IMEPELEKEA KUTOKUELEWA LUGHA HIZO MBILI VIZURI. AU UNASEMAJE. AHMED SALUM

      Delete
  10. MWAKYOSA SALOME TEKU BEL 101020
    KUTOKANA NA MABADILIKO KATIKA JAMII SERA YA LUGHA NAYO INAPASWA KUBADILIKA KULINGANA NA MABADILIKO YA JAMII KATIKA NYANJA ZOTE ZA MAISHA KAMA VILE KATIKA ELIMU, KISWAHILI KIWE NA HADHI SAWA NA LUGHA YA KIINGEREZA.KATIKA NCHI YA TANZANIA KWAKUA ZOTE NI LUGHA ZA KIOFISI.

    ReplyDelete
  11. MWAKYOSI SALOME TEKU BEL 101020
    KUTOKANA NA MABADILIKO KATIKA JAMII SERA YA LUGHA NAYO INAPASWA KUBADILIKA KULINGANA NA MABADILIKO YA JAMII KATIKA NYANJA ZOTE ZA MAISHA KAMA VILE KATIKA ELIMU, KISWAHILI KIWE NA HADHI SAWA NA LUGHA YA KIINGEREZA.KATIKA NCHI YA TANZANIA KWAKUA ZOTE NI LUGHA ZA KIOFISI.

    ReplyDelete
  12. KIFYULA ALEX TEKU/ BEL /10960
    Teaching professional is a professional where by we teachers should be fond of. A good teaching is not merely to impart information's to the student s but it is also to arouse the will of self -learning in them.The teacher should explore the interests ,attitudes,capacities ,competencies,and needs of the students and guid them accordingly.

    ReplyDelete
  13. MWAKALINGA TABEA.TEKU/BEL/101016 NIKWELI UKIANGALIA LUGHA ZIPO ZA AINA NYINGI NA PENGINE UNAWEZA UKAFIKIR KWA HARAKA KWAMBA IPITISHWE SERA KWA KUANGALIA LUGHA ZINGINE KAMA ILIVYO HAPO JUU,LAKINI MINAFIKIRI KAMA KISWAHILI NA KIINGEREZA NI TATIZO IWAJE KWA LUGHA ZINGINE, NAFIKIRI KUJIFUNZA LUGHA ZINGINE KAMA SOMO LINALOJITEGEMEA INATOSHA,MFANO KIFARANSA

    ReplyDelete
  14. PRESENTATION OF TED 501 MAKES ME TO BE AWARE WITH MEDIA TECHNOLOGY BECAUSE I LEARN MORE ABOUT IT. I KNOW HOW TO OPEN EMAIL,H0W TO RECORD AND TO KEEP DATA IN COMPUTER,TO USE PR0JECTOR. NYAMBO EKLESIA

    ReplyDelete
  15. ITS TRUE MADAM, TED 501 HELPS US MORE ABOUT MEDIA TECHNOLOGY. MWAKWENDA JENI

    ReplyDelete
  16. HIVI KISWAHILI NI LINI KITAKUWA LUGHA YA KUFUNDISHIA KATIKA VIWANGO VYOTE VYA ELIMU? KWANI KILA SIKU LIKO KWENYE MJADALA.
    KYALAMWENE KISSA

    ReplyDelete
    Replies
    1. NAHISI KWA JUHUDI ZETU WASOMI KUFANYA BIDII KUHAKIKISHA KISWAHILI KITUMIKE KUFUNDISHIA. JOSHUA ANGABILE

      Delete
  17. Inasikitisha sana kuona SPIKA wa MBUNGE kuunda TUME hati kuchunguza MITAHALA YA ELIMU ...!!!!

    Hii inaonesha jinsi gani kuna mitahala ya kila aina na kila shule yawezekana inafundisha kwa mtahala wake na mitahala hiyo ndiyo imetufikisha tulipo. HATARI SANA. Lakini WAZIRI WA ELIMU yupo, naibu wake, sio hawo tu, pia na katibu yupo mi sijui wanafanya nini, Labda mniambie. Kwanini wasiondolewe.
    Naomba nisiendelee kusema maana naumia.

    CHACHA JAMES. TEKU/BAED/10160

    ReplyDelete
    Replies
    1. SAWA NDUGU LAKINI KUKMBUKA ZOTE HIZI NI ATHARI ZA UKOLONI KWANI KATIBA TULIYONAYO NI KOPI YA KIKOLONI. HIVYO VIJANA TUANZE KUFANYA MABADILIKO NDUGU YANGU KWA KUWAWEKA VIONGOZI WENYE UZALENDO KAMA VILE WAZIRI MWAKYEMBE, MAGUFURI. MALEMBEKA GODFREY.

      Delete
  18. Watanzania tusiwe waoga wa kufanya mabadiliko.Hivi sasa tumejazwa hofu ya kwamba endapo tutakitumia Kiswahili kufundishia shule za msingi hadi vyuo vikuu,eti tutajiweka kuwa kisiwa dhidi ya ulimwengu wa nje.Hivi hawa viongozi wetu wa serikali wanaipeleka wapi sekta ya ELIMU Tanzania? Inaniuma sana!! Wakati huu kila mtanzania halisi anashuhudia jinsi kiwango cha ubora wa elimu nchini kilivyoshuka.Lakini kwa upande mwingine serikali inasema kiwango cha ubora wa elimu hakijashuka hata kidogo.Ama kweli!! Hapa hakuna utashi wa kisiasa.Je,mheshimiwa Raisi atakubali kuunda hiyo Tume? Na akiiunda itarudisha taarifa lini au ..............!! MHAPU YUWARD, TEKU/BAED/10476

    ReplyDelete
  19. NICODEMUS CHRISTOPHER TEKU /BEL /101042. Kiswahili kisipitishwe nchini tanzania kama lugha ya kufundishia kwa shule za sekondari na elimu ya juu kwasababu kina misamiati michache hususani katika ulimwengu huu wa saayansi na tekinolojia. lugha ya kiingereza inavyojitosheleza hivyo kiingereza kiendelee kutumika.

    ReplyDelete
  20. sera ya lugha yetu inaonekana kuwa ni dhaifu kutokana na utekelezaji duni,hivyo basi ili tuweze kuinua sera ya lugha yetu lazima utendaji na utekelezaji wa sera upewe kipaumbele. MWALIZI S LOYCE TEKU/BAED/10602

    ReplyDelete
  21. sera ya lugha yetu inaonekana kuwa ni dhaifu kutokana na utekelezaji duni,hivyo basi ili tuweze kuinua sera ya lugha yetu lazima utendaji na utekelezaji wa sera upewe kipaumbele. MWALIZI S LOYCE TEKU/BAED/10602

    ReplyDelete
  22. Ni kweli ni lazima tuwe na Tume ya yenye kuchunguza sera ya lugha ambayo kwayo itatusaidia kung`amua sera ya lugha kwa lugha mahsusi yenye kuwezesha na kutumika katika kufundishia,Tume husika itakayoundwa na Mheshimiwa Rais itakuwa ni chachu ya kuibua sera husika na kusababisha jamii kufaidika na matumizi ya lugha katika kujifunza.Na mimi naunga mkono hitimisho la Profesa Msanjila.

    Mgeta Matiku,Teku/Bel/10992.

    ReplyDelete
  23. NAKUBALIANA NA BW. MGETA ILA CHA KUJIULIZA MPK SASA TUME NGAPI ZIMEUNDWA NA BADO HAZIJAFNYIW KAZI?ILA KUMBUKA MABADILIKO YA UTUMIZI WA LUGH YA KISWAHILI YATALETWA NA SS WENYEWE WANA KISWAHILI

    SESEME SHABANI A
    TEKU/BEL/101066

    ReplyDelete
  24. WAO TUNAOWATEGEMEA WATUNGIZE KISW KIWE NDIO LUGHA YA KUFUNDISHIA NDIO HAOHAO WATOTO WAO WANAWPELEKA ENGLISH MEDIUM, HALAFU WAKIJA KWETU WANATUAMBIA TUTUMIE KISW, LKN CHA KUSIKITISHA ZAIDI WAO NDIO WADAU WENYEWE WANAOTEGEMEWA NA TAIFA KTK LUGHA HII NDIO WANAOTUANGUSHA , KUNA MSHAIRI MMOJA ANAITEWA SESEME KATIKA SHAIRI LAKE ANASEMA.

    Cha mwenzio si chako,chako ulicho nacho,
    Kiswahili lugha yako,ng’ang’ania lako jicho,
    Kwa kweli kina mashiko,dunia yatoa jicho(dunia yapiga jicho),
    Njooni watanzania kudumisha Kiswahili.


    ReplyDelete
  25. Hakika maneno ya katika hitimisho ya Profesa Msanjila yana umakini na ufundi ndani yake na yana uhalisia wa wakati tulionao,iwapo Rais pamoja na washauri wake watayazingatia haya,hakika tutakuwa na sera ya lugha yenye kugusa kila nyanja ya maisha ya Mtanzania wa leo na hata wa kesho.

    Kituka Nevizard, Teku / Baed / 10361.

    ReplyDelete
  26. Mimi naona matumizi ya kiingereza na kifaransa ni sahihi kabisa,na kufanya hivyo itatuwezesha sisi kama watanzania, hii yote ni kutoka na mahitaji ya sasa kwa suala zima la utandawazi,kwani itasaidia kuwasiliana na mataifa mbalimbali.

    Noah Rehema TEKU/BEL/101045

    ReplyDelete