Monday, January 28, 2013

Shairi: ASali Ya Afrika


Hili lilikuwa ni mojawapo ya Mashairi yaliyotakiwa kusomwa na Kughaniwa siku ya Kongamano,ila kutokana na muda halikupata nafasi ya kusomwa,lakini kwa juhudi za makusudi,tumekuletea hapa ulisome na kupata maudhui yake.....KARIBU SANA.



 ASALI  YA AFRIKA

                                                Lugha moja Afrika,                   si mpya bali asili,
                                                Ladha yake imefika,                  mdomoni sio kali,
                                                Kwa madaha kutamka,             uichezeapo akili,
                                                Ni asali Afrika,                           lugha tamu ya asili.

                                                Tumepita hatukwona,              Pwani hata milimani,
                                                Dunia tumeiona,                        hata ndani vilindini,
                                                Watu wanatazamana,               ikifika sikioni,
                                                Ni asali Afrika,                          utambapo kwa maneno.

                                                Asili yake Afrika,                      Pwani  yetu Mashariki,
                                                Tanzania yatukuka ,                 hata Kenya waafiki,
                                                Hata Ruanda imeruka ,            hakuna aliye dhiki,
                                                Ni asali Afrika,                          Burundi na hata Kongo.


                                                Umoja wa Afrika ,                    nao pia wakubali,
                                                Waonjapo wamefika,               utamu bila kabala,
Ulimi unahusika,                      ushahidi wakubali,
Ni asali Afrika,                          hasa huku Tanzania.


Wapo nguli Tanzania,                hakika tunawaenzi,
Shabani kwa yake nia,              Kiswahili alienzi,
Massamba alopania,                 kupandisha kurugenzi
Ni asali afrika,                            hao ndio kurugenzi.

Wapo wengine wengi,               kuwataja nachelea,
Wameandika kwa wingi,          nao hawajachelae,
Lugha yetu ya msingi,              kimapenzi inalea,
Ni asali Afrika ,                          kuiacha sitapenda.

Hakuna lugha  moja,                ya mawanda Afrika,
Mipaka si nchi moja,                robo yake Afrika,
Ndimi zao zimeonja,                 utamu uliotukuka,
Ni asali Afrika,                          hakuna lugha nyingine,.

Tanzania heko yako,                 kuienzi lugha yetu,
Hakika si peke yako,                na wengine si majitu,
Wanasifu mbele yako,              hawaachi huku kwetu,
Ni asali afrika,                            pembe yote Afrika.



Vyovyote Mashariki ,                lipo pale kama somo,
Teku chetu ndio hiki,                 tuna soma hili somo,
Na wengine waafiki ,                  kusaka utamu humo,
Ni asali Afrika ,                           hatuachi kutafuta.

Wahadhiri mahsusi,                  pomoni wamejuzika,
Taaluma yao  mahsusi ,            Kiswahili wanapika,
Wanazuoni wasusi,                    kwa lugha ilosukika
Ni asali Afrika ,                          njooni wote itayari.

Mbogela kamtazame.               Utadhani chomsiki,
Msamila usiseme,                     Kiswahili ni mziki,
Sekile hajawa kame,                 Fasihi kwake Batiki
Ni asali Afrika ,                         anatulisha Kamage.

Sijui tuseme nini,                     yenyewe mahanjumati
Ukila kaa pembeni,                 usije pigwa Manati
Gele zao zi pembeni,               kwa wengine hainati
Ni asali Afrika,                         njooni wote muilambe,




Imetayarishwa na 1.Chande Raphael TEKU/BEL/10917.

                              2. Nkwama Rutengamaso/TEKU/BEL/101044 .                                  

11 comments:

  1. ukweli kongamano la kiswahili lilifana sana,na maarifa mengi tumeyapata kuhusu sera ya lugha,hivyo ni jukumu letu sisi kama wana zuoni kuangalia mapungufu yaliyopo na tuyafanyie kazi ili kuleta mabadiliko katika sera ya lugha iliyopo.ndimi lwaho lucy TEKU/BAED/10399/GK.KWA PAMOJA TUNAWEZA KUFANYA MABADILIKO.

    ReplyDelete
  2. ni kweli ndugu sera ya lugha ina mapungufu mengi lakini haiwezi kuendelea mpaka imeingizwa katika mpango wa maendeleo ya taifa na kufanyiwa mabadiliko kulingana na mabadiliko na maendeleo ya jamii.FRANCIS HAPPY TEKU/BAED/10210/GK

    ReplyDelete
  3. KISWAHILI NI AZINA KWAMAENDELEO ENDELEVU

    (SESEME SHABANI A)

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ni kweli kaka lakini zingatia na huu utandawazi. je tutapata soko?
      MWAKANYAMALE PENDO

      Delete
    2. soko lazima lipatikane kwasababu kiswahili kitatumika katika idara zote. naungana na kaka seseme kwamba ni hazina kwa maendeleo endelevu.kiswahili juuu. ABASI SUBURA TEKU/BAED/10101

      Delete
  4. kiswahili chatuletea, maendeleo nchini,
    tabu imeshapotea, sasa tupo furahani,
    tuacheni mazoea, kujiweka dhalilini,
    kiswahil ni hazina ya afrika, kwa maendeleo endelevu.

    SEESEME SHABANI A
    TEKU/BEL/101066

    ReplyDelete
  5. KIBONA BAHATI TEKU/BAED/10342February 14, 2013 at 6:15 AM

    Kiswahili ni lugha ambayo inatakiwa iwe inatumika katika ngazi zote za elimu kama somo la kufundishia kwa sababu ni lugha inayo changia maendeleo.

    ReplyDelete
  6. Ni kweli kiswahili lugha itakayoleta maendeleo katika nchi za Afrika endapo kitapewa nafasi kama lugha ya kufundishia toka shule za msingi hadi vyuo vikuu. by NJOGOLO ELIZABETH TEKU/BAED/10697

    ReplyDelete
  7. Sasa kiswahili kipo juu kabisa kwani neno digital lapatiwa kiswahili fasaha.BAKITA wafumbua fumbo na kuita dijiti. hivyo kama kiswahili kitapewa nafasi kufundishia shule za msingi hadi vyuo, kitachangia maendeleo katika nchi yetu by KOMBA EDWARD A, TEKU/BAED/10366

    ReplyDelete
  8. Thanks very much Mama Mboya for your positive assistance about making interact through educational media and technology.
    SWENYA HONGERA
    TEKU/BAED/10821

    ReplyDelete
  9. Tanzania is not poverty country, because it is endowed with a varieties of resources.

    KINYUNYU MARIAM. M TEKU/BAED/10355

    ReplyDelete